Roman Abramovich ambaye ndiye mmiliki wa Chelsea amemfunga pingu Antonio Conte ndani ya Chelsea ambapo amepanga kutoruhusu kocha huyo kuachana na klabu hiyo.
Roman Abramovich ametoa agizo kwa viongozi wa Chelsea kuhusu kufanya haraka kumuongezea mkataba kocha huyo na mpaka sasa uongozi wa klabu hiyo umepanga kumpa mkataba mpya kocha huyo na utakaoongeza thamani ya mkataba huo toka £4.6milioni mpaka kufikia £7.2milioni.
No comments:
Post a Comment