Friday, 12 May 2017

Klopp; Liverpool ipo daraja moja na Chelsea

Kocha wa Liverpool, Jurgeon Klopp amesema anaamini katika daraja ambalo Chelsea yupo basi Liverpool nayo ipo japo imepitwa alama 14. Klopp ambaye anaiongoza Liverpool msimu huu ambayo inagombania nafasi nne za juu wakati Chelsea iliyochini ya Conte ikibakiza alama 3 kati ya michezo 3 iliyobaki kutangazwa kuwa bingwa mpya amesema bado Liverpool ina uwezo sawa na wakali hao wa London na hakuna tofauti yoyote baina ya timu hizo.

Liverpool ambayo imeshinda mchezo mmoja na kusuluhu mchezo mmoja msimu huu dhidi ya Chelsea imetetewa na Klopp na kusema ukitazama michezo waliyokutana timu hizo basi Liverpool haikuwa na tofauti kubwa kiuwezo na Chelsea.
"Rejea michezo waliyokutana timu hizo hakukuwa na tofauti ya kiuwezo lakini kama nilivyosema mafanikio ya Chelsea yamekuja kwa kuwa hawajapata majeruhi" alisema Klopp

"Akiumia Costa bado Hazard atacheza, akiumia Hazard bado Pedro na Willian watacheza na kufunga lakini pia sehemu ya ulinzi wao bado inakuwa imara kwa kuwa tu hawajapata majeruhi" aliongezea Klopp.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.