Thursday, 2 March 2017

We usimchezee Gavana

Yani kama kuna mtu akajaribu kumfananisha Diego Costa na washamba wengine kama Ibrahimovic basi huyo ni wa kupimwa akili.

Takwimu inaongea hakuna haja ya kupiga kelele....kulingana na ligi kuu Uingereza

Diego Costa vs Ibrahimovic
Michezo; Costa amecheza 24 na Ibrahimovic amecheza 24. Wote wapo sawa.

Dakika; katika michezo hiyo 24, Diego Costa amecheza dakika 2128 wakati Ibrahimovic katika michezo hiyo 24 amecheza dakika 2160. Ambapo Ki Ibrahimovic amecheza dakika nyingi kuliko Costa.

Magoli; Katika hiyo michezo yote Diego Costa amefunga magoli 16 wakati Ibrahimovic amefunga magoli 15. Kwa hiyo ingawa Ibrahimovic kacheza dakika nyingi kuzidi Costa lakini Costa kafunga magoli mengi zaidi.

Pasi za mwisho (Assist); Katika dakika hizo alizocheza Diego Costa ametoa pasi za mwisho 5 wakati Ibrahimovic ametoa pasi za mwisho 4. Kwa maana hiyo bado Costa ni bora zaidi ya Ibrahimovic.

Kadi za njano; wote wawili wamepata kadi za njano 5

Kadi nyekundu; wote wawili hakuna aliyepata kadi nyekundu.

Possession; Katika possesion Diego Costa ametengeneza 74.9% wakati Ibrahimovic ametengeneza 73.7%. Bado Costa kamzidi Ibrahimovic.

Rating; Diego Costa ana wastani wa 7.59 wakati Ibrahimovic ana 7.52. Bado Costa hajazidiwa

Hapana chezea huyu kiumbe Diego Costa a.k.a Gavana

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.