Wednesday, 1 March 2017

Koulibaly ni kama Uefa ndo itamleta Chelsea

Beki wa Napoli na timu ya taifa, Koulibaly aliyekuwa anatajwa kuhamia Chelsea anataka Uefa tu ili atue Chelsea.

Mtandao wa Goal unaamini beki huyo ataendelea kubaki Napoli endapo tu Napoli ikifuzu kucheza Uefa champions league kwa msimu ujao na kama haitofuzu itakuwa sababu kubwa ya ye kuondoka Italia.

Mchezaji huyo mwenye miaka 25 ambaye September 2016 alisaini mkataba mpya na timu hiyo ya Napoli, mkataba utakaomweka hapo mpaka 2021 anatajwa kuihama timu hiyo baada tu ya kutokufuzu ambapo mpaka sasa Napoli inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi kuu Italia na akiwa amewazidi wenzake kwa point chache tu akifukuziwa na timu kama Ac Milan na Inter Milan.

Ikumbukwe ligi kuu ya Italia itatoa timu 3 tu ili kufuzu kucheza Uefa msimu ujao. Kwa iyo kama Napoli atataka kufuzu basi asishuke alipo kwa sasa au apande kama akimaliza nafasi ya 4 kwenye ligi hatofanikiwa kufuzu.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.