Friday, 30 September 2016

3-5-2 inamfaa Alonso

Mfumo wa 3-5-2 ni mfumo ambao wachambuzi wa mpira huko majuu wameutaja kwamba ndio mfumo sahihi kuweza kumfanya Marcos Alonso acheze vizuri.

Maneno hayo yamesemwa na wachambuzi wa soka ambapo wameeleza katika mchezo uliopita wa ligi kuu uliowakutanisha wababe wa mji wa London, Arsenal dhidi ya Chelsea ambapo beki huyo ambae ni usajili mpya kutoka Fiorentina alipoingia kuchukua nafasi ya Fabregas timu ilionekana kuwa vizuri na mfumo huo ambapo baada ya kuingia yeye ndipo mfumo huo ulianza kutumika.

Lakini pia ikumbukwe taifa la Italia, timu nyingi katika nchi hiyo zinatumia mfumo huo na hata Conte kabla ya kuja England kipindi yupo Juventus timu kutoka Turin nchini Italia alikuwa anatumia mfumo huo, lakini pia Marcos Alonso ametokea Fiorentina ambayo pia ni timu kutokea huko Italia kwa hiyo inasemekana mfumo huo wa 3-5-2 utafaa kwa timu kwa kuwa kocha ndipo hesabu zake zilipo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.