Monday, 7 August 2017

PL; Siku 3 zimebaki

Siku 5 zimebaki kwa filimbi ya kwanza ya msimu mpya wa ligi kuu Uingereza maarufu kama Premier League kupulizwa.
Leo nitakuretea orodha ya wachezaji ambao Chelsea inatajwa kuwafukuzia ili kujiimarisha na msimu mpya.
Antonio Candreva, huyu ni winga wa Inter Milan anayetajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 25. Anatajwa kwa karibu kutua Chelsea mara baada ya Inter Milan kukiri ipo tayari kumuachia winga huyo mwenye miaka 30 kujiunga na Chelsea ili ipate fedha za kumsajili nyota mwengine.
Serge Aurier, huyu ni raia wa Ivory Costa, nchi anayotokea pia gwiji wa Chelsea, Didier Drogba. Aurier wa PSG anatajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 28 na Chelsea inatajwa kuipiku Man utd ambao wao wapo tayari kutoa paundi milioni 25 wakati Chelsea inaelezwa kuweka dau la paundi milioni 30.
Virgil van Dijk, mlinzi wa Southampton na raia wa Uholanzi. Huyu anatajwa kutoendelea kuwepp Southampton na Chelsea inatajwa kumuwania ingawa kuna upinzani mkubwa kutoka Liverpool.
Hao ni baadhi tu ya nyota wanaowaniwa na kocha Antonio Conte.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.