Nyota wa Chelsea, Willian siku ya leo anatimiza miaka 29, hapa nimekuwekea historia yake ya maisha haswa ndani ya Chelsea.
Jina kamili; Willian Borges Da Silva
Tarehe ya kuzaliwa; 09-Agosti-1988
Alipozaliwa; Ribeirao Pires, Brazil
Urefu; mita 1.7 (futi 5 na inchi 9)
Nafasi anayocheza; Winga au Kiungo mshambuliaji
Timu anayocheza; Chelsea
Namba ya jezi; 22
Tarehe ya kuzaliwa; 09-Agosti-1988
Alipozaliwa; Ribeirao Pires, Brazil
Urefu; mita 1.7 (futi 5 na inchi 9)
Nafasi anayocheza; Winga au Kiungo mshambuliaji
Timu anayocheza; Chelsea
Namba ya jezi; 22
Willian Borges alianza maisha yake ya soka akiwa na miaka 10 akiichezea klabu Corithians kama kinda aliyekuwa kwenye kulelewa kipaji chake, kabla ya kupandishwa mpaka timu ya wakubwa mwaka 2006 hapo akiwa na miaka 18. Aliichezea Corithians kwa mafanikio makubwa akiifungia magoli 2 kwenye michezo 20 kabla ya kutakiwa na kusajiliwa na Shaktar Donetsk kwa dau la Euro milioni 14 hapo akiwa na miaka 19.
Donetsk ilimjenga zaidi na kumtambulisha vyema nyota huyo ambapo hapo aliichezea klabu hiyo michezo 140 mengine ikiwa ya mechi za mabingwa wa Ulaya yaani mashindano ya klabu bingwa Ulaya maarufu kama Uefa, michuano iliyomtambulisha vyema na kuufanya moto wake uonekane. Aliifungia jumla ya magoli 20 katika michezo yote hiyo kabla ya kupokea ofa ya kujiunga na klabu ya Urusi ya Anzhi Makchachkala.
Alijiunga na Anzhi mwaka 2013 ambapo huko hakucheza sana baada ya kusumbuliwa na majeraha ambapo klabu hiyo aliichezea michezo 11 na kuifungia goli 1 tu na kupata ofa za kutoka nchini Uingereza.
Hapa sasa ndo watu watakumbuka vizuri juu ya uhamisho wake, ilionekana kabisa mchezaji huyu atajiunga na Tottenham na kila mtu akiamini hivyo ambapo alishafanyiwa vipimo na klabu hiyo ya jijini London, lakini wajanja wa Chelsea wakaipiga bao Tottenham na kuinasa saini yake huku kila mtu akishangazwa kwa umafia uliofanyika juu ya usajili wa nyota huyo.
Alisajiliwa na Chelsea kwa dau la paundi milioni 30 na kusaini mkataba wa miaka 5 kuichezea klabu hiyo yenye makazi yake magharibi mwa jiji la London. Hiyo ilikuwa tarehe 25-Agosti-2013.
Mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya FC Basel ambapo alishuhudia klabu yake ikipoteza katika mchezo huo kwa mabao 2-1. Kabla ya kucheza mchezo mwengine wa kwanza katika ligi kuu ambapo huo ulichezwa tarehe 06-Oktoba-2013 dhidi ya Norwich na mchezo huo uliisha kwa kushuhudia akiifungia goli la kwanza klabu yake hiyo.
Msimu wa 2014-2015 akiwa chini ya kocha Jose Mourinho aliiongoza vyema klabu hiyo kutwaa mataji mawili akishuhudia klabu hiyo ikitwaa Ligi Kuu Uingereza na kombe la Ligi wakati huo liliitwa Capital One.
Msimu uliofata ulikuwa mgumu kwa timu ambapo ulishuhudiwa Chelsea ikimaliza nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi huku ikitolewa mapema kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya na katika msimu huo Willian alicheza kwa kiwango cha hali ya juu na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa Chelsea.
Na msimu wa 2016-2017 ilitangazwa kwamba mchezaji huyo ameongeza mkataba wa miaka minne klabuni Chelsea kwa maana hiyo ikamaanisha mkataba wake utaisha 2022.
Kwa ujumla amecheza jumla ya michezo 460 na kufunga magoli 71 kwa ngazi ya klabu lakini kwa upande wa timu ya taifa ya Brazil amecheza michezo 45 na kuifungia magoli 7.
Maisha binafsi
Willian ni mme wa mke mmoja anayeitwa Vanessa Martins ambaye wamejaariwa kupata watoto mapacha wote wakike, Valentina na Manuella.
Willian ni mme wa mke mmoja anayeitwa Vanessa Martins ambaye wamejaariwa kupata watoto mapacha wote wakike, Valentina na Manuella.
Tarehe 13-Oktoba-2016 inaweza ikawa ndio siku mbaya kuliko zote kwa Willian maana ndiyo alimpoteza mama yake aliyefariki kwa ugonjwa wa kansa wakati huo Willian alikuwa Uingereza lakini aliruhusiwa kurudi nyumbani Brazil ili awepo kwenye mazishi ya mama yake.
Jambo usilolijua
Jambo usilolijua kwa Willian, mwaka 2014 alipohojiwa na chombo kimoja cha habari alisema "mi napenda kufurahi muda mwingi, napenda kutabasamu muda wote, kuna muda nafanya vituko ili kumfanya mwengine awe na furaha"
Jambo usilolijua kwa Willian, mwaka 2014 alipohojiwa na chombo kimoja cha habari alisema "mi napenda kufurahi muda mwingi, napenda kutabasamu muda wote, kuna muda nafanya vituko ili kumfanya mwengine awe na furaha"
Lakini pia alisema "Kama nisingekuwa nyota wa Chelsea basi ningekuwa kwetu Brazil nacheza kwenye kikundi cha samba"
Samba ni aina ya uchezaji mziki ambao ni maarufu sana nchini Brazil na ni kama utambulisho wa asili wa nchi hiyo, jinsi wanavyocheza nimekuwekea video yake.
![]() |
| Willian alipokuwa Shakter Donetsk |


No comments:
Post a Comment