Nyota wa kifaransa aliyeichezeaga Arsenal zamani, Thierry Henry ambaye kwa sasa anafanya kazi ya kuchambua soka ametoa neno juu ya usajili wa mshambuliaji mpya wa Chelsea, Alvaro Morata.
Henry alipohojiwa na Sky Sports alisema "ni wazi Chelsea imempata mtu sahihi, haswa usahihi wake unakuja kuwa chini ya Conte aliyewai kuwa naye pamoja Juventus"
"Itamchukua muda kidogo kuzoea mazingira na kuwa bora, lakini naamini kwa kuwa alishacheza chini ya Conte na akafanikiwa basi itakuwa hivyo akiwa Chelsea tena chini ya kocha yule yule" alisema Henry.
Alvaro Morata alisajiliwa na Chelsea katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha kubwa na mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo kadhaa huku akisaidia kutoa pasi ya mwisho kwa kichwa katika mchezo dhidi ya Inter Milan.

No comments:
Post a Comment