Wednesday, 9 August 2017

Conte atoa neno

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ametoa neno tena katika harakati za kukijenga kikosi kuelekea msimu mpya, ambao Chelsea itashiriki michuano kadhaa ikiwemo ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

Conte alisema "inatakiwa tujidhatiti na kufanya usajili sahihi na wa haraka kuelekea msimu mpya, itakuwa ngumu kwetu kufanya vizuri bila kufanya usajili"

Mpaka sasa Chelsea imeshafanikiwa kunasa saini za wachezaji wanne ambao ni Willy Caballero aliyechukuliwa bure akitokea Man city, kiungo mkabaji Tiemoue Bakayoko, mlinzi Antonio Rudiger na mshambuliaji Alvaro Morata.

"Ni wachezaji wazuri kuwasajili, lakini itakuwa vyema tukifanya mazoezi zaidi na kupambana sokoni" aliongeza Antonio Conte aliyeiongoza Chelsea kutwaa taji la ligi kuu msimu uliopita katika msimu wake wa kwanza akiwa kocha wa Chelsea.

Lakini pia kuna taarifa zimetoka kwamba msimamizi anayesimamia usajili wa Chelsea, mwanamama Glanovskaia ametoka klabuni kusafiri akizisaka saini za wachezaji wanaowaniwa na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.