Huenda hii ikawa ndio habari mbaya zaidi kwa wapenzi wa soka haswa wa Chelsea duniani kote. Haswa sisi Mashabiki wa Chelsea.
Winga na mshambuliaji wa Chelsea mwenye uraia wa Ubelgiji, Eden Michael Hazard huenda akaondoka klabuni hapo kabla hata ya pazia la usajili kufungwa usiku wa tarehe 31-Agosti.
Hiyo imeelezwa mara baada ya kudaiwa kuwepo mazungumzo ya chinichini juu ya kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane na mchezaji mwenyewe, Eden Hazard ikielezwa kwamba Hazard kamwambia kocha huyo kwamba kama akiifata Chelsea na kumtaka basi yeye kama Hazard atalazimisha kuuzwa ajiunge na mabingwa hao wa klabu bingwa Ulaya maarufu kama Uefa Champions League wa kihistoria.
No comments:
Post a Comment