Thursday, 24 August 2017

Conte kuondoka Chelsea?

Kumekuwa na taarifa za kumhusisha kocha wa Chelsea, Antonio Conte kwamba huweza akaondoka klabuni hapo. Lakini hapa nakupa taarifa za mwisho kuhusu habari hiyo na taarifa hizo zilizosambaa.

Ukweli ni kwamba hizo ni tetesi na zitabaki kuwa tetesi ambapo kocha huyo hatazamiwi kuondoka na ataendelea kubaki Chelsea. Hii ni kutokana na gazeti moja la nchini Uingereza.

Conte amekuwa akihusishwa na kuondoka klabuni hapo mara baada ya kudaiwa kwamba hana furaha klabuni hapo, na katika mkutano aliofanya na waandishi wa habari baada ya mchezo dhidi ya Burnley alikana na kusema ana furaha ndani ya Chelsea.

Kocha huyo muitaliano alikuja Chelsea msimu wa mwaka jana na kuisaidia kutwaa taji la ligi kuu.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.