Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ana mpango mzito wa kulilinda taji la ligi kuu na kufanya vizuri katika mashindano ya Ulaya na kuonyesha nia yake hiyo amempa kazi kiongozi wa Chelsea ambaye anashughulika kwenye usajili, Emenalo.
Kocha Conte amemwambia Emenalo afanye atakavyoweza ahakikishe Serge Aurier wa PSG anatua Chelsea na sio Man utd ambayo nayo inamuwania.
Conte anampango wa kuwasajili walinzi wawili ili kuziba pengo la walinzi na wachezaji walioondoka katika kipindi hiki cha usajili wakifikia wachezaji 17.
Conte alikasirishwa na kipigo cha juzi mara baada ya kupoteza tena katika fainali ya Ngao ya Hisani dhidi ya Arsenal na amepanga kuongeza wachezaji watatu.

No comments:
Post a Comment