Katika harakati za kocha Antonio Conte katika timu yake ya Chelsea bado anamipango kibao ya kukiimarisha kikosi. Kocha huyo wa Chelsea amepanga kukijenga zaidi kikosi cha Chelsea ambapo anatajwa kuwawania wachezaji mawinga watakaoweza kuwapa changamoto akina Marcos Alonso na Victor Moses.
Conte kwa sasa anatajwa kumuwania nyota Serge Aurier ambaye ni raia wa Ivory Coast ambayo ni nchi pia ya Didier Drogba, gwiji wa Chelsea.
Aurier anawaniwa pia na Man utd ambapo Chelsea inatajwa kutoa kiasi cha paundi milioni 30 wakati pia ikiiwania kwa karibu saini ya winga wa Italia na Inter Milan, Antonio Candreva

No comments:
Post a Comment