Chelsea siku ya leo mida ya mchana saa 14;35 itaingia tena uwanjani kupambana na mabingwa wa Ujerumani wenyeji wa jiji la Munich, Bayern Munich katika mchezo utakaopigwa barani Asia, katika jiji la Singapore katika uwanja wa Singapore National Stadium.
Mchezo huu unaweza kuwa mchezo wa kwanza kwa Alvaro Morata aliyesajiliwa na Chelsea kwa dau lililovunja rekodi klabuni hapo. Lakini winga Pedro Rodriguez hatokuwepo katika mchezo huu kutokana majeruhi aliyoyapata katika mchezo uliopita, na kwa sasa yupo London akiendelea na matibabu. Lakini pia Eden Hazard nae atakosekana.
Ila pia Kennedy ataukosa mchezo huu ambao Chelsea itaenda kumenyana na kocha wake wa zamani Carlo Ancelloti kutokana na mchezaji huyo kupata kashfa nzito juu ya ujumbe aliotuma mtandaoni akiwakashfu raia wa China wakati Chelsea ilipokuwa nchini humo.
No comments:
Post a Comment