Baada ya mshambuliaji mtukutu was Chelsea, Diego Costa kupokea taarifa kutoka kwa Antonio Conte kwamba haitajiki ndani ya The Blues na hayupo kwenye mipango yake kwa msimu ujao sasa kizaazaa hiki bado kinaendelea.
Unajua imekuwaje?
Baada ya Costa kusema kama kuondoka klabuni hapo basi sehemu anapotaka kwenda ni klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid lakini kukawa na kikwazo baada ya klabu hiyo kufungiwa kufanya usajili mpaka mwezi January mwaka 2018. Ikaonekana ili Costa aweze kuungana tena na klabu hiyo basi itambidi atafute klabu akacheze kwa mkopo huku akisubiri Atletico iweze kufutiwa adhabu yake kisha ndo aungane nayo.

Lakini sasa kocha wa klabu hiyo ya nchini Hispania, Diego Simeone ni kama amerahisisha mlolongo huo mara baada ya kusema Costa anaweza akaungana na Atletico Madrid lakini tu akiwa anafanya mazoezi na kikosi cha kwanza mpaka atakaposajiliwa mwezi January adhabu ya klabu hiyo itakapofikia kikomo. Bila kusajiliwa au hata kucheza mechi yoyote na klabu hiyo.
Diego Costa ambaye amekuwa mtu muhimu katika kikosi cha Chelsea, ambapo msimu uliopita amekuwa ndie mchezaji aliyefunga magoli mengi na kuisaidia Chelsea kuwa bingwa wa Ligi kuu mara 2 katika misimu mitatu aliyoitumikia klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment