Mshambuliaji kinda anayeichezea klabu mabingwa wa Scotland klabu ya Celtic, Moussa Dembele jioni ya leo ameipa kimuhemuhe cha aina yake klabu inayomfukuzia kwa karibu Chelsea pamoja na baadhi ya klabu nyengine kubwa za Ulaya ambazo zimeonesha nia ya kumtaka.
Dembele ametuma baadhi ya picha katika mtandao wa Instagram akiwaeleza mashabiki kwamba anafanya kikao maalumu na klabu ambayo hajaitaja jina, lakini pia akiwa na mabegi akionyesha yupo safarini kuelekea mahali ambapo hakutaka kupataja.
Haijajulikana kama anampango wa kuihama klabu hiyo aliyoifungia magoli 17 katika michezo 29 ya ligi ya Scotland au kama yupo safarini kujiunga na klabu nyengine. Lakini kama inakumbukwa vizuri mwezi January katika dirisha dogo la usajili mchezaji huyo pia alisemekana kusafiri kutoka Scotland na kwenda London ambapo inasemekana alifika kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.
Hizi ni baadhi ya picha alizozituma katika mtandao wa Instagram jioni ya leo.
No comments:
Post a Comment