Kutokana na gazeti moja la nchini Hispania inaelezwa Chelsea inaongoza katika mbio za kumuwania nyota wa Real Madrid, James Rodriguez ambapo inaelezwa Chelsea ipo tayari kutoa £70milioni.
James Rodriguez anaonekana hana nafasi katika kikosi hicho haswa ambapo Real Madrid inatajwa kumuwania kwa karibu nyota wa Monaco, Kylian Mbappe. Lakini pia kwa Antonio Conte anatafuta saini ya mchezaji huyo kwa karibu baada ya kuikosa saini ya Alvaro Morata ambaye amekubali kutua Man utd.
No comments:
Post a Comment