Kati ya makocha bora na wenye heshima Uingereza, Harry Redknapp amesema alishangazwa na Conte alivyoanza kwa kutua walinzi wanne badala ya mfumo wake uliozoeleka ambao alikuwa akiutumia pindi alipokuwa Juventus na timu ya taifa ya Italia.
Kocha Antonio Conte alifika Chelsea muda mfupi baada ya kuachana na timu ya taifa ya Italia na alipofika Chelsea alikuwa akitumia mfumo wa walinzi au mabeki wanne nyuma na katika michezo 6 ya kwanza alifanikiwa kupata alama 10 kati ya 18 ambazo angezipata kama angeshinda michezo yote hiyo 6. Lakini baada ya kupokea kipigo kizito kutoka kwa Arsenal ndipo kocha huyo akaamua kuutumia mfumo ambao alishauzoea.
Harry Redknapp amesema "nilishangaa kuona Conte hakucheza kama alivyocheza hivi leo maana alianza kwa mfumo tofauti na ule ambao aliuzoea"
No comments:
Post a Comment