Kiungo mshambuliaji wa Arsenal mwenye uraia wa Chile, Alexis Sanchez ambaye amekuwa na msimu mzuri ndani ya Arsenal na ligi kuu ya Uingereza kwa ujumla amefichua kwamba anatamani sana kuichezea Chelsea.
Maneno hayo aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Daily star na kufichua ni kweli alikuwa na maisha ya furaha ndani ya Arsenal lakini kwa sasa hali imegeuka na anatamani kung'atuka katika klabu hiyo ambayo imekuwa na msimu mbovu baada ya kutolewa katika klabu bingwa ya Ulaya maarufu kama Uefa Champions league kwa jumla ya magoli 10-2 na wababe wa Ujerumani, Bayern Munchen na hapo hapo kutokuwa na uhakika wa kufuzu kucheza mashindano hayo ya ulaya baada ya mpaka sasa wiki ya 32 ikishika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.
"Ni kweli nilikuwa na maisha ya furaha ndani ya Arsenal, ila kama hii shati yangu (akionyesha fulana yake nyeusi aliyoivaa wakati wa mahojiano) wakati naivaa ilikuwa inanipendeza na kunitosha vizuri lakini itafikia kipindi haitonipendeza tena na kunitosha. Kwa maana hiyo sitoihitaji tena" alisema Sanchez,
"kutua Chelsea ni jambo ambalo siwezi kuliepuka, napenda na natamani litokee" aliongeza
Ikumbukwe nchini mwake (Chile) ambapo mchezaji huyo anapendwa na kuheshimika kutokana na anavyoipambania timu yake hiyo ya taifa, wananchi walianzisha maandamano kumshawishi shujaa wao huyo, Sanchez aweze kuihama timu hiyo ya Arsenal maana wamechoka kumuona shujaa wao akimaliza misimu kadhaa na klabu hiyo yenye makao yake London kaskazini bila kuwa na mataji. Na maandamano hayo yalihimizwa baada tu ya kulipotiwa Sanchez alisafiri kwenda mbali na timu yake siku moja baada ya kipigo cha goli 5-1 na kutupwa nje ya mashindano ya Uefa Champions hali ambayo ilielezwa ni kutokana na maelewano mabovu na kocha wake, Arsene Wenger.
Lakini pia klabu hiyo ya Arsenal inaonekana kutopendezwa na nia ya kumuuza mchezaji huyo baada ya kumpa ofa kubwa ya mkataba mpya utakaompa Sanchez £300,000 (paundi 300,000).
No comments:
Post a Comment