Uwanja wa Chelsea wa Stamford Bridge umepewa baraka za kutosha na meya wa jiji la London ulipo uwanja huo.
Uwanja huo ambao kwa sasa unaingiza jumla ya mashabiki 40,000 umepangwa kufanyiwa matengenezo ili kuupanua na kutarajiwa kuingiza jumla ya mashabiki 60,000 pamoja na kuboreshwa ili kuwa wa kisasa zaidi.
Uwanja huo ambao ni uwanja pekee kuwai kutumika na Chelsea toka kuanzishwa kwake mwaka 1905 umepangwa kufanyiwa matengenezo yatakayosababisha Chelsea kutoutumia uwanja huo ndani ya misimu mitatu ya ligi kuu Uingereza au zaidi ya hapo. Na meya wa jiji la London amepongeza mpango huo na kusema;
"hili ni jambo zuri, Chelsea ni klabu kubwa duniani. Na watu wengi wanaitazama. Kupanuliwa kwa kiwanja chake inamaana itawakaribisha wengi kufika London" alisema Sadiq Khan
Matengenezo hayo yanatajwa kuwa na thamani ya £500milioni (paundi milioni 500) na unategemewa kumalizika mwaka 2021 huku ukithimamiwa na kampuni iliyotengeneza uwanja wa Allianz Arena ule unaotumiwa na timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munchen.
No comments:
Post a Comment