Leo usiku katika jiji la London katika uwanja wa London stadium kutakuwa na mchezo wa timu zinazotoka katika jiji moja la London yaani West Ham united watakaomenyana na Chelsea FC au watoto wa Abramovic.
Mchezo huo ambao utakaopigwa kwa masaa ya Afrika mashariki itakuwa saa 23:00 usiku utazikutanisha timu hizo ambapo kwa mchezo wa kwanza ambao ulichezwa kwa raundi ya kwanza kabisa ambao nao ulichezwa jumatatu siku kama ya leo, Chelsea walishinda 2-1 kabla ya kukutana tena katika mchezo wa kombe la ligi na West Ham kurudisha 2-1.
Kwa upande wa West Ham watawakosa baadhi ya wachezaji kama mfungaji wao bora Michail Antonio aliyeifungia timu hiyo magoli 8 msimu huu, lakini pia beki wao Ogbonna naye watamkosa. Lakini kizuri ni kwamba wana matumaini makubwa kwa Andy Carroll kucheza mchezo huo baada ya kupata majeruhi.
Ila kwa upande wa Chelsea ni Hazard pekee aliyejigonga na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini lakini haijathibitishwa kama ataukosa mchezo wa leo.
No comments:
Post a Comment