Saturday, 4 March 2017

Refa wa video kutumika FA Cup msimu ujao

Chama cha soka cha nchini Uingereza FA ambacho pia kinasimamia mashindano ya kombe la FA nchini umo limeleta teknolojia mpya ndani ya mashindano ya FA Cup itakayoanza kufanyika msimu ujao katika hatua ya raundi ya tatu mpaka mchezo wa fainali wa kombe hilo.

Chama hicho ambacho kimeamua kutumia refa video katika mashindano yake ya msimu ujao kuanzia raundi ya tatu.

Refa video ndio nini?
Ni mfumo mpya ambao unatumia mfumo wa kamera ya video ili kumuonyesha mwamuzi kama atakuwa na wasiwasi na maamuzi au tendo lililotokea uwanjani.

Refa wa kati kama atakuwa labda hajaona tendo lililotokea uwanjani kabla ya kulitolea maamuzi au hana uhakika na maamuzi yake basi ataenda pembeni ya uwanja ambapo kutakuwa na Tv na kuangalia kwa umakini kwa kile kilichotokea na ndipo afanye maamuzi sahihi.

Mfumo huo ambao unakuja baada ya mfumo wa Goal Technology kutambulishwa na kuanza kutumika katika ligi za Uingereza unaonekana utasaidia sana kwa mwamuzi kutoa maamuzi ambayo yana uhakika na ya haki kwa 100%.

Mmoja wa viongozi wa chama hicho cha soka cha Uingereza, FA wakati anatambulisha kuhusu teknolojia hiyo alisema
"tunaamini ni teknolojia nzuri na itatufaa sana kwa kuwa imeshatumika katika baadhi ya maeneo kwa maana hiyo nasi tutajifunza kutoka kwao"

Refa video kutumika kombe la dunia 2018
Lakini pia mfumo huo umetambulishwa kutumika pia katika kombe la dunia la mwaka 2018 na uongozi wa chama cha mpira wa miguu duniani, FIFA.

Mabadiliko manne
Lakini pia msimu huo wa mwaka kesho kuna sheria mpya itatumika katika sehemu ya kufanya mabadilisho ya mchezaji yaani kufanyiwa substations ambapo inategemewa kufanyika mara nne kwa timu moja katika mchezo mmoja. Yaani kama timu ikicheza na ikamaliza idadi yake ya kubadilisha mchezaji ambayo kwa kawaida ni mara tatu alafu mkafikia katika dakika 30 za nyongeza basi ile timu itaruhusiwa kutoa mchezaji wa nne kama kukamilisha sheria iyo. Nayo inategemewa kutumika msimu huo wa 2017-2018.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.