Kuelekea katika wiki ya 27 ya ligi kuu ya Uingereza katika mchezo wa wababe katika mji mmoja yaani wote wa London kati ya West Ham itakayowakaribisha Chelsea katika uwanja wa London Stadium.
Kama ilivyokawaida nakuletea historia ya mchezo huu na taarifa zote za kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa jumatatu ya tarehe 06-March-2017 katika mishale ya saa 23:00 (saa 5:00 usiku)
Historia
West Ham na Chelsea kwa mara ya kwanza zimekutana tarehe 20-October-1923 mchezo ambao Chelsea alikuwa nyumbani Stamford Bridge ambapo ulishuhudiwa na mashabiki 51000 katika michuano ya ligi daraja la kwanza na mchezo huo ukaisha kwa kutoshana nguvu kwa sare ya 0-0.
Na mchezo wa mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa tarehe 26-October-2016 ambapo ilikuwa katika mashindano ya kombe la ligi la EFL na West Ham kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa London Stadium ulioingiza mashabiki 45,957.
Takwimu
Kwa takwimu toka kuanzishwa kwa timu hizo na kukutana katika mashindano mbalimbali wamekamilisha jumla ya michezo 107 na Chelsea kufanikiwa kushinda michezo 48 na kufungwa michezo 39 na kutoka suluhu michezo 20.
Michezo iliyopita
Katika ngazi ya ligi kuu Uingereza hizi ndio matokeo yao ya mwisho ndani ya msimu huu wa 2016-2017
Chelsea-Ameshinda michezo 3 na kutoa suluhu michezo 2 kwa maana hiyo katika michezo 5 amefanikiwa kuvuna alama 11 kati ya alama 15.
West Ham-Ameshinda michezo 2 na kufungwa 1 huku akitoa suluhu michezo 2 kwa maana hiyo katika michezo 5 amefanikiwa kuvuna alama 8 kati ya alama 15.
Wachezaji watakaokosekana
Chelsea-Hakuna atakayekosekana
West Ham-Watawakosa wachezaji Ogbonna, Diafro Sakho na Gokhan Tore ingawa pia kwa Andy Carroll haijathibitishwa kama atakuwepo
Utamu wa mchezo huu
1. Huu ndo mchezo wa kwanza kati ya timu hizi kukutana katika uwanja wa London Stadium kwa mwaka huu
2. Chelsea imepoteza michezo miwili tu kati ya michezo 21 iliyopita ya ligi kuu Uingereza dhidi ya West Ham. Imeshinda michezo 21, Chelsea imeshinda 15 na kusuluhu michezo 4.
3. Mchezo wa mwisho kwa Chelsea na West Ham kukutana kwa mara ya mwisho matokeo yalikuwa West Ham kutoka na ushindi wa 2-1 katika kombe la EFL. Katika uwanja wa London Stadium.
4. Conte na Chelsea yake imepoteza michezo miwili tu kati ya mitatu aliyocheza ugenini dhidi ya timu za London ambapo alipoteza kwa Arsenal mwezi September na Tottenham mwezi January na kutoa kuifunga Crystal Palace.
5. Andy Carroll ambaye ni mshambuliaji wa West Ham ameifunga Chelsea mara 2 kati ya mara 3 walipokutana.
6. Cesc Fabregas wa Chelsea ana jumla ya pasi za mwisho 102 ambazo alizitimiza katika mchezo uliopita ambao pia ulikuwa mchezo wake wa 300 katika ligi kuu Uingereza akihitaji assist moja tu ili awe mchezaji wa pili mwenye pasi za mwisho nyingi ndani ya ligi kuu Uingereza. Kwa sasa ana pasi za mwisho sawa na Frank Lampard mwenye pasi za mwisho 102.
7. Lanzini wa West Ham amezifunga timu za London mara 7 katika michezo 11 aliyokutana nazo. Ana magoli 7 dhidi ya timu za London.
8. Diego Costa wa Chelsea anahitaji magoli 2 ili awe mchezaji wa tano kwa ligi ya Uingereza kwa kufikisha magoli matano kwa haraka. Hawa ndio waliofunga magoli 50 kwa haraka
>Andrew Cole kwa michezo 65
>Alan Shearer kwa michezo 66
>Ruud Van Nistelrooy kwa michezo 68
>Fernando Torres kwa michezo 72
Wakati Diego Costa kwa sasa ana magoli 48 kwa michezo 78.
No comments:
Post a Comment