Jina kamili; David Luiz Moreira Marinho
Tarehe ya kuzaliwa; 22-April-1987
Miaka yake; 29
Mahali alipozaliwa; Diadema, Brazil
Urefu; meta 1.89 (futi 6 na inchi 2½)
Nafasi anayocheza; Mlinzi wa kati au kiungo mkabaji
Klabu anayochezea; Chelsea
Namba; 30
Timu ya taifa; Brazil
David Luiz ambaye alikuwa anatumia jina la mchezaji nyota wa zamani wa Brazil, Kaka kwa kuwa alikuwa anampenda sana alianza soka lake akiwa na miaka 4 katika klabu ya Sao Paulo ya nchini kwao Brazil na mpaka 2001 kuhamia klabu ya Vitoria ambayo aliichezea mpaka mwaka 2007 wakati huo akiwa na miaka 20.
Baada ya hapo ndipo alipopelekwa kwa mkopo katika klabu ya Benfica ambapo baada ya msimu wake mmoja kuisha klabu hiyo ilipendezwa na kiwango chake ndipo ikamsajili moja kwa moja.
Aliichezea Benfica michezo 82 na kuifungia magoli 4 kabla ya Chelsea iliyokuwa chini ya boss wa kirusi kuipelekea maombi klabu hiyo ya Benfica kwamba walikuwa wanamtaka Luiz lakini watamtoa na Matic pamoja na ela ili kubadilishana na ndipo Luiz kwa mara ya kwanza akazivaa jezi za Chelsea mgongoni akiwa na namba 4. Hiyo ilikuwa mwaka 2011.
Katika maisha yake ndani ya Chelsea alifanikiwa kutwaa kombe la klabu bingwa ya Ulaya maarufu kama Uefa na kombe la FA na akafanikiwa kuichezea michezo 81 na kuifungia magoli 6, na kuuzwa tena kwenda Ufaransa katika klabu ya P.S.G mwaka 2014 usajili ambao uliweka rekodi ya kuwa mlinzi aliyesajiliwa kwa dau kubwa la £50milioni (paundi milioni 50).
Alicheza P.S.G kwa mafanikio mpaka alipofanikiwa kutwaa nayo mataji manne ya Ufaransa mpaka pale August 2016 aliporudi tena Chelsea.
Mpaka sasa Luiz anaichezea Chelsea na mpaka sasa ameshaichezea michezo 25 na kuifungia goli 1 katika mchezo dhidi ya Liverpool.
Na kwa timu ya taifa ya Brazil aliichezea mwaka 2007 katika timu ya Brazil U20 na kuichezea michezo 2 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa na kufanikiwa kuichezea michezo 55 na kuifungia magoli 3 na mwaka 2013 kufanikiwa kutwaa nayo taji la FIFA Confederation Cup na pia kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 2014.
Usilolijua kuhusu huyu jamaa, alibatizwa mwaka 2015 akiwa P.S.G katika bwawa la kuogelea la mchezaji mwenzake Maxwell.
No comments:
Post a Comment