Tuesday, 7 March 2017

Hazard; Ni kama pacha wangu

Nyota wa mchezo baina ya West Ham dhidi ya Chelsea wa jana usiku, Eden Hazard amemsifia mchezaji mwenzake, N'Golo Kante ambaye amekuwa na kiwango cha hali ya juu toka alipotua Uingereza katika klabu ya Leicester city akitokea Caen ya Ufaransa.

"namuona sehemu yote uwanjani. Uwanja mzima utamkuta. Namuona kulia, namuona kushoto, kucheza nae najiona kama nacheza na pacha wangu" alisema Hazard akimsifia Kante.

Eden Hazard aliyekuwa nyota wa mchezo huo alifunga goli la mapema dakika ya 25 kabla ya nyota mwengine wa Chelsea, Diego Costa kufunga goli jengine kipindi cha pili kabla ya kushuhudia West Ham wakichomoa goli moja dakika za majeruhi katika dakika ya 93. Goli lililofungwa na Lanzini.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.