Tuesday, 7 March 2017

David Luiz anatisha

Mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa amestaafu soka, Frank Lampard amemuongelea mlinzi wa kati ambaye kwa sasa anaichezea kwa mafanikio klabu yake ya sasa, Chelsea.
"David (Luiz) amepevuka sana kwa sasa. Anaonyesha ukomavu. Kipindi kile wakati alipoondoka kwenda PSG alikuwa na tatizo la kufanya makosa lakini toka amerudi anaonyesha ukomavu na anacheza kwa jitihada sana. Navutiwa nae." alisema Frank Lampard.

David Luiz ambaye alirudi Chelsea baada ya kuuzwa PSG kwa kuvunja rekodi ya kuwa mlinzi aliyesajiliwa kwa £50milioni (paundi milioni 50) alirudi Chelsea muda mfupi kabla ya dirisha la usajili kufungwa na mpaka sasa katika michezo 27 iliyocheza Chelsea katika ligi kuu imeruhusu magoli 18 tu na ye akiwa imara katika ukuta huo mnene.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.