Friday, 30 September 2016

Loftus Cheek: Lampard ni noma

Kiungo na zao la academy ya Chelsea ambaye kiwango chake kipo juu kwa sasa kwa makinda wa Chelsea, Loftus Cheek ametoa sifa kuhusiana na Lampard.

Alisema "katika maisha yangu ya soka na katika kulipenda soka nilikuwa navutiwa na kutamani kuwa kama Frank Lampard" akaongezea "alikuwa na kipindi kibora akiwa hapa na amebaki kuwa role model kwangu"

Ikumbukwe Lampard ndiye mchezaji aliyewai kutokea Chelsea na kuwa mfungaji bora wa muda wote ndani ya klabu hiyo akiwa na magoli zaidi ya mia mbili. Akiwa kabeba pia mataji kadhaa kama ligi kuu, klabu bingwa ulaya n.k.

Kwa sasa Lampard anacheza katika ligi kuu ya Marekani.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.