Chelsea imekuwa ikitajwa juu ya kuongeza wachezaji wenye uraia wa Uingereza klabuni hapo ikiwa pia ikitajwa kutaka kuimarisha kikosi kujiweka sawa na mashindano au michuano ambayo klabu hiyo inashiriki. Kati ya wachezaji wa kiingereza waliokuwa wanatajwa na Chelsea ni winga wa Arsenal, Alex Oxlade Chamberlain na sasa kuna habari mpya juu ya mchezaji huyo aliyekataa kusaini mkataba mpya ndani ya timu ya kocha Arsene Wenger.
Habari zilizopo zinadai kwamba Arsenal ipo tayari kumuuza Chamberlain aliyebakiza mwaka mmoja klabuni hapo kumuuza kwenda Chelsea na siyo kwenda Liverpool ambayo nayo imetajwa kumuwania.
Arsenal inaona ni bora mchezaji huyo akajiunga na Chelsea ambayo yenyewe ipo kugombania taji la ligi kuu kuliko kumuuza kwenda Liverpool ambayo yenyewe inatajwa kuwa adui wa Arsenal juu ya nafasi ya nne yaani Top Four ya Uingereza.

No comments:
Post a Comment