Sunday, 6 August 2017

Ngao ya Hisani; Chelsea yapoteza tena kwa Wenger

Leo ni siku nyengine mbaya kwa Antonio Conte baada ya siku kadhaa kutimiza miaka 48 lakini leo ameishuhudia klabu yake ikipoteza tena kwa kocha mfaransa, Arsene Wenger katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo kwa dakika 90 mchezo huo uliisha kwa sare ya moja kwa moja ambapo Chelsea ilipata goli la kuongoza dakika chache baada ya kutoka mapumziko goli likifungwa na Victor Moses kabla ya kushuhudia Pedro Rodriguez akicheza rafu mbaya iliyomshuhudia akitolewa kwa kadi nyekundu. Baada ya kucheza rafu hiyo ndiyo iliyosababisha Kolasinac mlinzi mpya wa Arsenal kuchomoa goli kwa kichwa murua.

Goli hilo lilifanya mpaka mchezo huo kuisha kwa sare hiyo na kuzishuhudia timu hizo zikifika matuta.

Ndipo ule mfumo mpya wa matuta ukaanza kutumika, mfumo wa ABBA ambapo wa kwanza kupiga alikuwa mchezaji nahodha wa Chelsea, Gary Cahill aliyepiga vizuri na kufunga. Akafatiwa na mchezaji wa Arsenal, Oxlade Chamberlain aliyeifungia timu hiyo kwa tuta kabla ya Monreal kufunga tena. Baada ya hapo golikipa wa Chelsea Thibaut Courtois akapiga tuta ambalo lilipaa mbali na goli na kuifanya Arsenal kuongoza kwa matuta 3 kwa 1. Alvaro Morata naye akapiga akakosa, na hivyo kuifanya Arsenal kuwa na nafasi kubwa ambapo giroud alikuja kumaliza kazi kwa kupiga tuta tamu lililofanya Arsenal kushinda mchezo huo kwa matuta 4 kwa 1.

Kwa mchezo huu umemfanya Antonio Conte kushuhudia akipoteza michezo miwili ya fainali mbele ya kocha Arsene Wenger na Arsenal yake.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.