Zimebaki siku mbili kufungwa kwa dirisha kubwa la usajili ambapo litafungwa usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa ya wiki hii, ambapo itakuwa siku ya tarehe 31-Agosti. Na mpaka sasa Chelsea imekuwa ikihusishwa na wachezaji kadhaa licha ya mpaka sasa kuwasajili nyota watatu ambao ni Alvaro Morata, Antonio Rudiger na Tiemoue Bakayoko na Willy Caballero aliyekuja bure mara baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Man city.
Mpaka sasa Danny Drinkwater anatajwa kwa karibu kuja Chelsea akitokea Leicester city. Na kwa habari zilizopo ni kwamba Chelsea imesema ipo tayari kutoa dau la paundi milioni 25 ingawa wao Leicester wanataka kumuuza nyota huyo raia wa Uingereza mwenye miaka 27 kwa dau la paundi milioni 40.

No comments:
Post a Comment