Wednesday, 9 August 2017

Conte bado na Ox

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte bado anampango wa kuongeza wachezaji katika kikosi chake kujiandaa na msimu mpya, msimu ambao utakuwa na michezo mingi haswa kukiwa na michuano mikubwa ya klabu bingwa Ulaya ambapo Chelsea itashiriki pia.

Alex Oxlade Chamberlain ni mchezaji mmojawapo anayefukuziwa na Chelsea ambapo kikosi hicho kina mpango wa kuongeza wachezaji wazawa kikosini hapo ambapo kwa kikosi cha kwanza cha Chelsea kuna mchezaji mzawa mmoja tu ambaye ni Gary Cahill.

Chelsea imeshaweka mezani kiasi cha paundi milioni 25 ilichokitenga ili kumsainisha jamaa huyo anayeichezea Arsenal iliyomsajili kutokea Southampton.

Chamberlain alitengewa na klabu yake kiasi cha paundi 100,000 ili asaini mkataba mpya wakati mkataba wake wa sasa unaisha mwezi wa 6 mwakani

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.