Cesc Fabregas amekuwa mchezaji anayeng'aa sana haswa akipewa nafasi. Hajatumiwa sana na Antonio Conte msimu huu lakini mara anapopewa nafasi anacheza kwa kiwango cha hali ya juu.
Hizi ndizo takwimu za Fabregas tokaalipotua Chelsea, na huwa inatokea vipi kama akiwepo au asipokuwepo.
Toka ametua Chelsea mwezi August mwaka 2011 imechezwa michezo 102 ye akiwa mchezaji rasmi wa Chelsea. Na katika michezo hiyo ye amecheza 88 na ambayo hakucheza ni michezo 14.
Katika michezo 88 aliyocheza timu imefanikiwa kufunga magoli kwa wastani wa 1.8 na wakati katika michezo ambayo hajacheza timu ilifunga magoli kwa wastani wa 1.7
>kwa hiyo inaonyesha ana wastani mzuri wa kuisaidia timu kufunga magoli
Katika michezo aliyocheza, katika timu kufungwa magoli, katika michezo aliyocheza timu imefungwa magoli kwa wastani wa 1.4 kwa kila mechi wakati katika michezo ambayo hakucheza timu ilifungwa magoli kwa wastani wa 0.4
>kwa maana hiyo kuwepo kwake katika timu inasababisha timu kuruhusu magoli mengi
Katika michezo ambayo amecheza katika timu timu imetoka ikiwa na ushindi kwa 56% wakati katika michezo ambayo hajacheza yaani yupo benchi basi timu inakuwa na uhakika wa kuondoka na ushindi kwa 86%
No comments:
Post a Comment