Najua kuna mengi hujapata kuyajua kuhusu ukubwa na historia ya uwanja unaotumiwa na Chelsea kama uwanja wake wa nyumbani, Stamford Bridge.
Jina kamili;
Stamford Bridge
Unapatikana;
Fulham katika jiji la London katika nchi ya Uingereza
Umefunguliwa; 28-April-1877
Idadi ya mashabiki; 41,663
Kuingiza mashabiki wengi;
82,905 katika mchezo wa Chelsea vs Arsenal mwaka 1935
Ukubwa wa uwanja;
mita 103×67 (yadi 112.6×73.2)
Kampuni iliyokitengeneza;
Archibald Leitch
Jina Stamford Bridge limetoka katika jina Stamfordesbrigge ikimaanisha "The Bridge of Sandy Ford"
Uwanja wa Stamford Bridge umewai kutumiwa na klabu moja ilikuwa inaitwa London Athletic Club ambayo ndio klabu ya kwanza kuutumia uwanja huo, walianza kuutumia kuanzia mwaka 1877 mpaka mwaka 1904 ambapo hapo kabla ulikuwa upo chini ya Joseph Mears kabla ya mdogo wake Gus Mears alipopata wazo la kuanzisha klabu yake mpya ya Chelsea ambapo ndo ikaanza rasmi kuutumia uwanja huo.
Lakini pia klabu ya mchezo wa rugby ya London Monarchs ilishawai kuutumia uwanja huo mwaka 1997.
Uwanja huo ni kati ya viwanja ambavyo vina historia kubwa nchini Uingereza ambapo ni mmoja kati ya viwanja vikongwe kuanza kuanzishwa mapema kabisa na ni kiwanja cha 8 kwa ukubwa kati ya viwanja vinavyotumika katika ligi kuu Uingereza msimu huu.
Lakini pia uwanja huu umeundwa na sehemu nne ambazo zimejitenga kama majukwaa. Majukwaa hayo yametenganishwa kwa majina ili kuleta tofauti;
1. Mathew Harding Stand
Hili jukwaa mwanzo lilikuwa linaitwa North Stand ambalo lilipewa jina la Mathew Harding Stand kwa kuwa kulikuwa na mmoja wa viongozi wa Chelsea aliyeitwa Mathew Harding ambaye alisaidia maendeleo ya klabu na maendeleo wa uwanja na alifariki 22-October-1996 katika ajali ya ndege ndogo (helicopter). Jukwaa hilo linachukua jumla ya mashabiki 10,884 waliokaa.
2. East Stand and Shed End
Jukwaa hili linachukua jumla ya mashabiki 11,000.
3. Shed End
Jukwaa hili ndilo jukwaa ambalo lina viti vichache, yani hili jukwaa ndio maalumu ya wale mashabiki wa kuhamasisha sana yani wao wapo radhi washangilie huku ngoma zikipigwa kwa muda wote ndo maana wao hawana haja ya kukaa chini wao wapo radhi wasimame muda wote. Hili jukwaa mwanzoni lilikuwa linaitwa Fulham Road End lakini mashabiki wakalibatiza jina hilo la Shed End na ndipo uongozi nao ukaliendeleza. Jukwaa hili lina viti 6,414.
4. West Stand
Jukwaa hili linachukua jumla ya mashabiki 13,500
Lakini pia uwanja huu wa Stamford Bridge umekuwa ukitumika na timu ya taifa ya England kwa kucheza baadhi ya michezo yake, na katika michezo yake yote iliyocheza katika uwanja huu haijawai kupoteza mchezo wowote.
Mwaka 1909, Uingereza ilimbamiza Uholanzi magoli 9-1.
Mwaka 1913, Uingereza ikamfunga jirani yake Scotland goli 1-0.
Mwaka 1929, Uingereza ilimbamiza jirani yake mwengine Wales magoli 6-0.
Mwaka 1932, Uingereza ilimfunga Austria 4-3.
Mwaka 1946, Uingereza tena ikamlamba Switzerland 4-1.
Mwaka 2013, safari hii ilikuwa Brazil ikatoka suluhu na Urusi magoli 1-1.
Michezo yote hiyo ni ndani ya Stamford Bridge.
Na jengine kama haujajua, Stamford Bridge uwanja unaotumika na Chelsea ndio uwanja mkongwe kuliko viwanja vinavyotumiwa na timu zote kubwa za Uingereza.
Old Trafford, uwanja unaotumiwa na Man utd umefunguliwa 1910.
Anfield unaotumiwa na Liverpool umefunguliwa 1884.
City of Manchester unaotumiwa na Man city umefunguliwa 2003
Emirates stadium unaotumiwa na Arsenal ulifunguliwa 2006 lakini kabla ya hapo Arsenal walikuwa wanautumia Highbury ambao nao ulifunguliwa 1913
White Hart Lane uwanja unaotumiwa na Tottenham Hotspur ulianzishwa au kufunguliwa 1899.
Wakati uwanja wa Stamford Bridge unaotumiwa na Chelsea ulifunguliwa 1877.
No comments:
Post a Comment