Mlinzi wa Juventus ambaye alikuwa akihusishwa na kuungana na kocha wake wa zamani Antonio Conte waliokuwa wote Juventus na timu ya taifa ya Italia, Leonardo Bonnuci amesema yeye hana mipango ya kuihama timu yake hiyo ya mjini Turin na mipango aliyokuwa nayo ni mikubwa na anataka kubaki hapo. Labda kama kwa kwenda Chelsea basi labda Juventus waamue wao kumuuza.
Bonnuci ambaye hakuweza kujumuishwa katika kikosi kilichomenyana na FC Porto katika mchezo wa hatua ya 16 bora wiki kadhaa zilizopita kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na kocha wake wa sasa wa Juventus, Allegri na ikasemekana kwa sababu hiyo itamfanya kuachana na timu hiyo lakini baadae Bonnuci alimfata Allegri na kumuomba radhi kwa lililotokea. Na sasa amerudishwa katika kikosi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment