Beki mwenye uraia wa Senegal ambaye kwa sasa anaichezea Napoli ya Italia, Kalidou Koulibaly ambaye amekuwa akihusishwa kwa namna kubwa kutua Chelsea, inaonekana ana uwezekano mkubwa wa kutua darajani msimu ujao.
Kwanini atue?
Koulibaly ambaye ana umri wa miaka 25 anatazamiwa kuwa mbadala kwa safu ya ulinzi ya Chelsea kwa msimu ujao ambapo David Luiz atakuwa anauelekea uzee kwa kuwa mpaka sasa ana umri wa miaka 29 wakati ukuta wa sasa unamtegemea sana yeye pamoja na Gary Cahill ambaye naye haonekani kuwa imara sana kwa msimu ujao. Azpilicueta bado ana umri unaoruhusu kucheza zaidi.
Nathan Ake na Kurt Zouma wakiwa nje kuangalia wataingia wapi katika 3-4-3 lakini Conte anamtazamia Koulibaly kama atakuwa mtu sahihi wa kucheza kama beki wa kati.
Koulibaly ambaye mpaka sasa ameichezea Napoli jumla ya michezo 30 na huku akifunga goli moja katika michezo yote hiyo anatazamiwa kuwa ndo usajili mkubwa kwa Conte kuutaka kuufanya ili kulifanya eneo la ulinzi kuwa imara zaidi.
Koulibaly anatajwa kuwa na thamani ya £30milioni (paundi milioni 30) kiasi ambacho kinatajwa kuwa kikubwa katika kumnunua beki ingawa kuna baadhi ya wachambuzi wanaona ni heri arudishwe Christensen aliye kwa mkopo Borrusia Monchenglbech.
No comments:
Post a Comment