Baada ya ushindi wa goli 1-0 wa Chelsea ulioupata mbele ya Manchester utd, hizi ndizo rekodi zilizowekwa katika mchezo huo
1. Chelsea kwa sasa haijafungwa michezo 12 mfululizo iliyocheza dhidi ya Manchester utd katika mashindano yote. Chelsea imeshinda 7 na kutoa sare michezo 5.
2. Lakini pia, rekodi hiyo imefanya Chelsea kutokufungwa na muda mrefu ambapo mara ya mwisho kwa Chelsea kufungwa na Manchester utd ilikuwa mwaka 2012. Wengine waliokuwa na rekodi ya kutokufungwa na Manchester utd kwa muda mrefu ni Liverpool mwaka 1927 ambapo haikufungwa kwa mechi 13, na Leeds mwaka 1972 ambaye naye hakufungwa michezo 13.
3. Kushinda kwa Chelsea katika mchezo huo wa robo fainali kumefanya jiji la London kuingiza timu 3 katika nusu fainali ambazo ni Chelsea, Arsenal na Tottenham. Mara ya mwisho kufanyika kitu kama hicho ilikuwa mwaka 2002 ambapo ziliingia Chelsea, Arsenal na Fulham.
4. Manchester utd wamekuwa na uwezo wa kucheza mpira au kutawala mpira (ball possession) ndogo kabisa katika msimu huu katika mchezo mmoja. Ball possession ya 26%.
5. Chelsea imefika nusu fainali mara 22. Wanaoongoza kwa kufika nusu fainali ni Arsenal aliyefika mara 29, Manchester utd mara 28, Everton mara 26, na Liverpool mara 24.
No comments:
Post a Comment