David Luiz amesema katika maisha yakebya soka anatamani siku moja arudi klabu yake ya zamani ya Benfica ambayo ndio ilikuwa klabu yake ya kwanza kuichezea ndani ya bara la Ulaya.
"natamani kurudi Benfica, natamani kumalizia soka langu huko. Ilikuwa ngumu sana kwenye mchezo wa fainali mwaka 2013 (Chelsea ilipocheza fainali ya Europa league na Benfica na Chelsea kufanikiwa kutwaa kombe) niliumia nilipowaona marafiki zangu wakiwa na huzuni"
Beki huyo mwenye uraia wa Brazil alisajiliwa na Chelsea akitokea Benfica ambapo Chelsea walitoa hela pamoja na mchezaji (Nemanja Matic) ili kumpata beki huyo kisiki ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 29.
No comments:
Post a Comment