Mchana wa leo kama ilivyo kawaida ya Antonio Conte amefanya tena mkutano kabla ya mchezo dhidi ya West Ham hapo jumatatu. Na haya ndio aliyoyasema.
Kuhusu tetesi za yeye kwenda Inter Milan
Conte; nafikiri jambo langu lipo wazi. Kama unataka kujaribu kutengeneza kitu chochote basi unategemea utakuwa nacho kwa baadae pia. Hilo lipo wazi
*akimaanisha yupo Chelsea ili kutengeneza timu atakayokuwa nayo kwa muda mrefu zaidi
Kuhusu familia
Conte; Jambo pekee naloweza kusema kuhusu familia yangu ni kwamba inanihitaji. Wao wapo Italia wakati mi natengeneza klabu ya baadae lakini nitawaleta ili tuwe karibu mimi na wao
Kuhusu West Ham
Conte; ni timu nzuri na wanacheza vizuri. Walitufunga mara ya mwisho katika kombe la EFL nadhani ni timu nzuri na inayotaka matokeo. Lakini mimi na timu yangu tutaendelea kupambana ili tuweze kupata alama 3.
Kuhusu Andy Carroll
Conte; ni mchezaji mzuri na mwenye nguvu pia. Nitaifanya timu yangu tuwe nae makini kumzuia yeye pamoja na timu kwa ujumla.
Kuhusu Batshuayi
Conte; Ni mchezaji mzuri anayejaribu kucheza kwa bidii ili aonyeshe uwezo wake.
Kuhusu maheruhi
Conte; kikubwa hakuna majeruhi ya moja kwa moja. Ni Hazard tu aliumia jumatano kwenye mazoezi lakini sio kama ni majeruhi kabisa, ilikuwa kawaida tu.
Kuhusu mkataba wake
Conte; kila kocha anapofika kwenye timu anataka akae muda mrefu, aisaidie timu iweze kupata matokeo mazuri lakini inapotokea kama yaliyomtokea Ranieri basi ndo inabidi uwe tayari kwa yote.
Kuhusu mkataba mpya wa Moses
Conte; Anastahili. Ni mchezaji mwerevu, anapigana na anayetaka mafanikio muda wote. Nilipomuona kwenye mechi za kujiandaa na msimu mpya nikaona huyu atanifaa zaidi.
No comments:
Post a Comment