Je unajua mechi baina ya West Ham dhidi ya Chelsea wamekuwa na matokeo ya kufanana msimu huu?
Timu hizo zimekutana mara tatu ndani ya msimu huu wa 2016-2017 na mchezo wa kwanza walicheza katika uwanja wa Stamford Bridge na Chelsea kutoka na ushindi wa 2-1.
Baada ya hapo zikakutana tena katika kombe la EFL na zikakutana katika uwanja wa London Stadium na wakaifunga Chelsea magoli 2-1.
Na jana ya tarehe 06-March wamekutana tena na Chelsea imeshinda 2-1.
Yaani katika michezo mitatu waliyokutana imeisha kwa idadi sawa ya magoli. Katika michezo hiyo Chelsea imeshinda michezo 2 na kufungwa na 1.
Chelsea imefunga magoli 5 katika michezo hiyo 3 na kufungwa magoli 3.
No comments:
Post a Comment