Kocha wa West Ham united, Slaven Bilic ametoa neno kuelekea mchezo wa leo.
"ninapoiongelea Chelsea naiona kama timu tofauti, wanacheza kwa nguvu, wanapigana, wanatumia kila mbinu kuhakikisha wanatoka na ushindi. Wanatumia mfumo wa mabeki watatu japo kiukweli wanakaba watano."
akaongeza "embu waangalie Moses na Alonso. Wanacheza kama walinzi viungo (wing-backs) wanatafuta mpira na wanashambulia. Wamekuwa ni zaidi ya mawinga. Timu nzima inasaka mpira na inakaba kwa nguvu, labda Costa ndo huwa hakabi kidogoo na Hazard."
West Ham leo itaikaribisha Chelsea katika uwanja wake wa nyumbani wa London Stadium mishale ya saa 5 usiku ndio timu zitakuwa zinaingia uwanjani.
No comments:
Post a Comment