Kiongozi wa Barcelona alikuwa kwenye jukwaa la viwanja vya London Stadium siku ya jumatatu katika mchezo wa West Ham dhidi ya Chelsea ambapo Chelsea ilishinda 2-1. Katika mchezo huo ambao kiongozi huyo wa Barcelona inasemeka alifika hapo ili kuwaangalia Matic, Azpilicueta na Marcos Alonso ili kuweza kuwasajili kwa maana kwa sasa timu hiyo wababe wa Hispania wamebadilisha mfumo na kwa sasa wanatumia 3-4-3 ambao pia unatumiwa pia na Chelsea ambapo umewapatia matokeo mengi chanya mpaka kufikia sasa.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la The Sun la Uingereza limeeleza kwa kuwa Chelsea iliamua kubadili mfumo wake na kutumia mfumo wa 3-4-3 imepata mafanikio sana na kwa maana hiyo Barcelona ambayo nayo imeingia katika mfumo huo wanaamini wanaweza kupata wachezaji sahihi katika mfumo huo kutoka Chelsea maana ni muda sasa toka timu hiyo kuutumia mfumo huo.
No comments:
Post a Comment