Monday, 26 September 2016

Di Maria chini ya Conte kwa mikono ya Luiz

Mchezaji Angel Di Maria amebainisha anatamani kurudi EPL ambapo alianza kabla ya kutimkia PSG. Angel Di Maria alisajiliwa na PSG akitokea Man utd ambapo kwa sasa hana furaha kucheza mahali hapo chini ya maboss wa kiarabu.
Kauli hiyo inaweza ikawa furaha kwa Conte ambapo mtu wake wa karibu alinukuliwa akisema kati ya wachezaji ambao Conte anawahusudu kwa soka lao safi na la ufundi basi Di Maria ni mmoja wapo ambapo kwa kauli hiyo ya Di Maria inatakiwa imshtue Conte ili kuweza kumleta darajani.
Lakini pia usisahau kwamba kipenzi cha wengi pale PSG haswa kwa wachezaji alikuwa ni David Luiz ambae kwa sasa ni mchezaji wetu kwa iyo nadhani na naamini pia uwepo wa Luiz Chelsea unaweza ukatumika kama chambo kwa Angel kutua The Blues

1 comment:

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.