Nyota wa Chelsea, Diego Costa ambaye ameonyeshwa mlango wa kutokea na kocha wake Antonio Conte huwenda akakamilisha ndoto na nia yake ya kujiunga na klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
Hiyo inaweza kutokea muda wowote kuanzia sasa ambapo ripoti zinasema Atletico ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 41. Diego Costa ambaye ni mshambuliaji bora katika kikosi kilichobeba ubingwa waUIngereza msimu uliopita alipokea ujumbe kutoka kwa Antonio Conte akiambiwa hayupo kwenye mipango ya Chelsea na badala yake ajindae kufungasha virago.
Diego Costa ameshakataa ofa za timu kadhaa ambazo zimekuwa zikimuania mara baada ya kuonyeshwa mlango. Timu ambazo zilipeleka maombi kwa mchezaji huyo ni kama AC Milan, Everton na klabu kadhaa kutoka China.
No comments:
Post a Comment