Danny Drinkwater bado anaendelea kuwatoa udenda Chelsea na mashabiki wote wa Chelsea dunia nzima. Huenda muda wowote nyota huyo mwenye miaka 27 akaungana na nyota wa Chelsea, N'golo Kante ambaye kabla walishacheza wote timu moja wakiwa Leicester city kabla ya Kante kuamia Chelsea.
Drinkwater analazimisha kuondoka Leicester akitaka ajiunge Chelsea, mpango ambao Leicester wanautilia ngumu mara baada ya kukataa ofa ya Chelsea ambayo ipo tayari kutoa paundi milioni 27 ingawa wao Leicester wanataka kiasi cha paundi milioni 30.
Chelsea ina upungufu wa wachezaji raia wa Uingereza ambapo kwenye kikosi cha kwanza kuna raia wa Uingereza mmoja tu ambaye ni Gary Cahill ambaye pia anaweza akapoteza nafasi katika kikosi cha kwanza muda wowote, na kisheria za nchi ya Uingereza ambapo timu hiyo inapatikana inakataza klabu kutokuwa na mchezaji hata mmoja wa nchini humo kwa maana hiyo Chelsea inasaka wachezaji wa kiingereza ambapo mpaka sasa inatajwa kuwafukuzia nyota kama Ross Barkley, Oxlade Chamberlain, Jamie Vardy na Danny Drinkwater.